← Psalms (150/150) |
1. | Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake. |
2. | Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. |
3. | Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi; |
4. | Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi; |
5. | Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana. |
6. | Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya. |
← Psalms (150/150) |