← Psalms (146/150) → |
1. | Haleluya. |
2. | Nitamsifu Bwana muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai. |
3. | Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake. |
4. | Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea. |
5. | Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, Na tumaini lake ni kwa Bwana, Mungu wake, |
6. | Aliyezifanya mbingu na nchi, Bahari na vitu vyote vilivyomo. Huishika kweli milele, |
7. | Huwafanyia hukumu walioonewa, Huwapa wenye njaa chakula; Bwana hufungua waliofungwa; |
8. | Bwana huwafumbua macho waliopofuka; Bwana huwainua walioinama; Bwana huwapenda wenye haki; |
9. | Bwana huwahifadhi wageni; Huwategemeza yatima na mjane; Bali njia ya wasio haki huipotosha. |
10. | Bwana atamiliki milele, Mungu wako, Ee Sayuni, kizazi hata kizazi. Haleluya. |
← Psalms (146/150) → |