← Psalms (142/150) → |
1. | Kwa sauti yangu nitamlilia Bwana, Kwa sauti yangu nitamwomba Bwana dua. |
2. | Nitafunua mbele zake malalamiko yangu, Shida yangu nitaitangaza mbele zake. |
3. | Nilipozimia roho uliyajua mapito yangu; Katika njia niendayo wamenifichia mtego. |
4. | Utazame mkono wa kuume ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho. |
5. | Bwana, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katika nchi ya walio hai. |
6. | Ukisikilize kilio changu, Kwa maana nimedhilika sana. Uniponye nao wanaonifuatia, Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi. |
7. | Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu. |
← Psalms (142/150) → |