← Psalms (136/150) → |
1. | Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
2. | Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
3. | Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
4. | Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
5. | Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
6. | Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
7. | Yeye aliyefanya mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
8. | Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
9. | Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
10. | Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
11. | Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
12. | Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
13. | Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
14. | Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
15. | Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
16. | Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
17. | Yeye aliyewapiga wafalme wakuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
18. | Akawaua wafalme mashuhuri; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
19. | Sihoni, mfalme wa Waamori; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
20. | Na Ogu, mfalme wa Bashani; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
21. | Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
22. | Urithi wa Israeli mtumishi wake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
23. | Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
24. | Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
25. | Kila chenye mwili akipa chakula chake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
26. | Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
← Psalms (136/150) → |