← Psalms (133/150) → |
1. | Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja. |
2. | Ni kama mafuta mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake. |
3. | Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko Bwana alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele. |
← Psalms (133/150) → |