← Psalms (127/150) → |
1. | Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure. |
2. | Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi. |
3. | Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu. |
4. | Kama mishale mkononi mwa shujaa, Ndivyo walivyo wana wa ujanani. |
5. | Heri mtu yule Aliyelijaza podo lake hivyo. Naam, hawataona aibu Wanaposema na adui langoni. |
← Psalms (127/150) → |