← Psalms (125/150) → |
1. | Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele. |
2. | Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele. |
3. | Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki; Wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu. |
4. | Ee Bwana, uwatendee mema walio wema, Nao walio wanyofu wa moyo. |
5. | Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, Bwana atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli. |
← Psalms (125/150) → |