← Psalms (111/150) → |
1. | Haleluya |
2. | Matendo ya Bwana ni makuu, Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo. |
3. | Kazi yake ni heshima na adhama, Na haki yake yakaa milele. |
4. | Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu; Bwana ni mwenye fadhili na rehema. |
5. | Amewapa wamchao chakula; Atalikumbuka agano lake milele. |
6. | Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake, Kwa kuwapa urithi wa mataifa. |
7. | Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu, Maagizo yake yote ni amini, |
8. | Yamethibitika milele na milele, Yamefanywa katika kweli na adili. |
9. | Amewapelekea watu wake ukombozi, Ameamuru agano lake liwe la milele, Jina lake ni takatifu la kuogopwa. |
10. | Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana akili njema, Sifa zake zakaa milele. |
← Psalms (111/150) → |