← Job (8/42) → |
1. | Ndipo Bildadi huyo Mshuhi akajibu, na kusema, |
2. | Wewe utanena maneno haya hata lini? Maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo mkuu hata lini? |
3. | Je! Mungu hupotosha hukumu? Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki? |
4. | Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi, Naye amewatia mkononi mwa kosa lao; |
5. | Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi; |
6. | Ukiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa. |
7. | Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana. |
8. | Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani, Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta; |
9. | (Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno, Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;) |
10. | Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza, Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao? |
11. | Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matope Na makangaga kumea pasipo maji? |
12. | Yakiwa yakali mabichi bado, wala hayakukatwa, Hunyauka mbele ya majani mengine. |
13. | Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu; Na matumaini yake huyo mbaya huangamia; |
14. | Uthabiti wake utavunjika, Na matumaini yake huwa ni nyuzi za buibui. |
15. | Ataitegemea nyumba yake, isisimame; Atashikamana nayo, isidumu. |
16. | Yeye huwa mti mbichi mbele ya jua, Nayo machipukizi yake huenea katika bustani yake. |
17. | Mizizi yake huzonga-zonga chuguu, Huangalia mahali penye mawe. |
18. | Lakini, aking'olewa mahali pake, Ndipo patamkana, na kusema, Mimi sikukuona. |
19. | Tazama, furaha ya njia yake ni hii, Na wengine watachipuka kutoka katika nchi. |
20. | Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu, Wala hatawathibitisha watendao uovu. |
21. | Bado atakijaza kinywa chako kicheko, Na midomo yako ataijaza shangwe. |
22. | Hao wakuchukiao watavikwa aibu; Nayo hema yake mwovu haitakuwako tena. |
← Job (8/42) → |