← Job (36/42) → |
1. | Tena Elihu akaendelea na kusema, |
2. | Ningojee kidogo nami nitakueleza; Kwa kuwa nikali na maneno kwa ajili ya Mungu. |
3. | Nitayaleta maarifa yangu kutoka mbali, Nami nitampa haki Muumba wangu. |
4. | Kwani yakini maneno yangu si ya uongo; Aliyekamilika katika maarifa yu pamoja nawe. |
5. | Tazama, Mungu ni hodari, wala hamdharau mtu ye yote; Ana uweza katika nguvu za fahamu. |
6. | Hauhifadhi uhai wa waovu; Lakini huwapa wateswao haki yao. |
7. | Yeye hawaondolei macho yake wenye haki; Lakini pamoja na wafalme huwaweka Katika viti vya enzi milele, nao hutukuzwa. |
8. | Nao wakifungwa kwa pingu, Wakitwaliwa kwa kamba za mateso; |
9. | Ndipo huwaonyesha matendo yao, Na makosa yao, ya kuwa wametenda kwa kujivuna. |
10. | Yeye huyafunua masikio yao, wasikie maonyo, Na kuwaagiza warudi kuuacha uovu. |
11. | Kama wakisikia na kumtumikia, Watapisha siku zao katika kufanikiwa, Na miaka yao katika furaha. |
12. | Lakini wasiposikia, wataangamia kwa upanga, Nao watakufa pasipo maarifa. |
13. | Lakini hao wasiomcha Mungu mioyoni hujiwekea hasira Hawalilii msaada hapo awafungapo. |
14. | Wao hufa wakali vijana, Na uhai wao huangamia katikati ya wachafu. |
15. | Yeye humponya aliyetaabika kwa njia ya taabu yake, Na kuyafunua masikio yao kwa maonevu. |
16. | Naam, yeye angekuongoza utoke katika msiba Hata mahali penye nafasi, ambapo hapana msonge; Na kilichowekwa mezani pako kingejaa mafuta. |
17. | Lakini umejaa hukumu ya waovu; Hukumu na haki hukushika. |
18. | Basi ujitunze, isije hasira ikakuvuta hata ukafanya mzaha; Wala usikubali ukuu wa ukombozi ukugeuze. |
19. | Je! Mali yako yatatosha, hata usiwe katika taabu, Au uwezo wote wa nguvu zako? |
20. | Usiutamani usiku, Wakati watu wakatwapo katika mahali pao. |
21. | Jitunze, usiutazame uovu; Kwani umeuchagua huo zaidi ya taabu. |
22. | Tazama, Mungu hutenda makuu kwa uweza wake; Ni nani afundishaye kama yeye? |
23. | Ni nani aliyemwagiza njia yake? Au ni nani awezaye kusema, Wewe umetenda yasiyo haki? |
24. | Kumbuka kuitukuza kazi yake, Watu waliyoiimbia. |
25. | Wanadamu wote wameitazama; Watu huiangalia kwa mbali |
26. | Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui; Hesabu ya miaka yake haitafutiki. |
27. | Kwani yeye huvuta juu matone ya maji, Yamwagikayo katika mvua kutoka kungeni mwake; |
28. | Ambayo mawingu yainyesha Na kudondoza juu ya wanadamu kwa wingi. |
29. | Naam, mtu aweza kuelewa na matandazo ya mawingu, Ngurumo za makao yake? |
30. | Tazama, yeye huutandaza mwanga wake, umzunguke; Naye hufunika vilindi vya bahari. |
31. | Kwani huwahukumu kabila za watu kwa njia hizi; Hutoa chakula kwa ukarimu. |
32. | Yeye huifunika mikono yake kwa umeme; Na kuuagiza shabaha utakayopiga. |
33. | Mshindo wake hutoa habari zake, Anayewaka hasira juu ya uovu. |
← Job (36/42) → |