← Job (35/42) → |
1. | Tena Elihu akajibu na kusema, |
2. | Je! Wewe wadhani kwamba haya ni haki yako, Au je! Wasema, Haki yangu ni zaidi kuliko ya Mungu, |
3. | Maana wasema, Kutakuwa na faida gani kwako wewe? Tena, Nitapata faida gani, kuliko nikifanya dhambi? |
4. | Mimi nitakujibu, Na hawa wenzio pamoja nawe. |
5. | Ziangalie mbingu ukaone; Na mawingu yaangalie, yaliyo juu kuliko wewe. |
6. | Ikiwa umefanya dhambi, umefanya nini juu yake? Yakiwa makosa yako yameongezeka, wamfanyia nini yeye? |
7. | Ikiwa u mwenye haki, wampa kitu gani? Au yeye hupokea nini mkononi mwako? |
8. | Uovu wako waweza kumwumiza mtu kama wewe; Na haki yako yaweza kumfaa mwanadamu. |
9. | Kwa sababu ya wingi wa jeuri wao hulia; Walilia msaada kwa sababu ya mkono wa wakuu. |
10. | Wala hapana asemaye, Yuko wapi Mungu Muumba wangu, Awapaye nyimbo wakati wa usiku; |
11. | Atufundishaye zaidi ya hayawani wa nchi, Na kutufanya wenye hekima kuliko ndege za angani? |
12. | Hulia huko, lakini hapana ajibuye, Kwa sababu ya kiburi cha watu waovu. |
13. | Hakika Mungu hatasikia ubatili, Wala Mwenyezi hatauangalia. |
14. | Sembuse usemapo wewe ya kuwa humwangalii, Hiyo daawa i mbele yake, nawe wamngojea! |
15. | Lakini sasa, kwa sababu yeye hakukujilia katika hasira zake, Wala hauangalii sana unyeti; |
16. | Ndiposa Ayubu hufunua kinywa chake kwa ubatili; Huongeza maneno pasipo maarifa. |
← Job (35/42) → |