← Job (25/42) → |
1. | Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema, |
2. | Enzi na hofu zi pamoja naye; Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka. |
3. | Je! Majeshi yake yahesabika? Ni nani asiyetokewa na mwanga wake? |
4. | Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu? Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke? |
5. | Tazama, hata mwezi hauangazi, Wala nyota si safi machoni pake; |
6. | Siuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu! |
← Job (25/42) → |