← Job (11/42) → |
1. | Ndipo Sofari Mnaamathi akajibu, na kusema, |
2. | Je! Huu wingi wa maneno usijibiwe? Na mtu aliyejaa maneno, je! Ahesabiwe kuwa na haki? |
3. | Je! Majivuno yako yawanyamazishe watu wawe kimya? Nawe hapo ufanyapo dhihaka, je! Hapana mtu atakayekutahayarisha? |
4. | Kwa kuwa wewe wasema, Mafunzo yangu ni safi, Nami ni safi machoni pako. |
5. | Lakini, laiti Mungu angenena, Na kuifunua midomo yake juu yako; |
6. | Tena akuonyeshe hizo siri za hekima, Ya kuwa hufanikiwa katika kuyatimiza makusudi yake! Ujue basi ya kuwa Mungu akuachilia katika uovu wako. |
7. | Je! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikilia upeo wa huyo Mwenyezi? |
8. | Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe? |
9. | Cheo chake ni kirefu kuliko dunia, Ni kipana zaidi ya bahari. |
10. | Yeye akipita, na kufunga watu, Na kuwaita hukumuni, ni nani basi awezaye kumzuia? |
11. | Kwani yeye awajua watu baradhuli; Huona na uovu pia, hata asipoufikiri. |
12. | Lakini mpumbavu aweza kupata ufahamu, Ingawa mwanadamu huzaliwa kama mtoto wa punda-mwitu. |
13. | Wewe ukiuweka moyo wako kwa uelekevu, Na kumnyoshea mikono yako; |
14. | Ikiwa una uovu mkononi mwako, uweke mbali nawe, Wala usikubali upuzi kukaa hemani mwako; |
15. | Hakika ndipo utakapopata kuinua uso pasipo ila; Naam, utathibitika, wala hutakuwa na hofu; |
16. | Kwa kuwa utasahau mashaka yako; Utayakumbuka kama maji yaliyokwisha pita; |
17. | Na maisha yako yatakuwa meupe kuliko adhuhuri; Lijapokuwa ni giza, litakuwa kama alfajiri. |
18. | Nawe utakuwa salama, kwa sababu kuna matumaini; Naam, utatafuta-tafuta kando yako, na kupumzika katika salama. |
19. | Tena utalala, wala hapana atakayekutia hofu; Naam, wengi watakutafuta uso wako. |
20. | Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho. |
← Job (11/42) → |