← Job (10/42) → |
1. | Nafsi yangu inachoka na maisha yangu; Sitajizuia na kuugua kwangu; Nitanena kwa uchungu wa roho yangu. |
2. | Nitamwambia Mungu, Usinihukumie makosa; Nionyeshe sababu ya wewe kushindana nami. |
3. | Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuyaangazia mashauri ya waovu? |
4. | Je! Wewe una macho ya kimwili, Au je! Waona kama aonavyo binadamu? |
5. | Je! Siku zako ni kama siku za mtu, Au je! Miaka yako ni kama siku za mtu, |
6. | Hata ukauliza-uliza habari za uovu wangu, Na kuitafuta dhambi yangu, |
7. | Ujapojua ya kuwa mimi si mwovu; Wala hapana awezaye kuokoa na mkono wako? |
8. | Mikono yako imeniumba na kunifinyanga; Nawe utageuka na kuniangamiza? |
9. | Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo; Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena? |
10. | Je! Wewe hukunimimina kama maziwa, Na kunigandisha mfano wa jibini? |
11. | Umenivika ngozi na nyama, Na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa. |
12. | Umenijazi uhai na upendeleo, Na maangalizi yako yameilinda roho yangu. |
13. | Lakini mambo haya uliyaficha moyoni mwako; Najua kuwa haya yamo nafsini mwako; |
14. | Nikifanya dhambi, ndipo waniangalia, Wala hutaniachilia na uovu wangu. |
15. | Mimi nikiwa mbaya, ole wangu! Nami nikiwa mwenye haki, walakini sitainua kichwa changu; Mimi nimejaa aibu Na kuyaangalia mateso yangu. |
16. | Kichwa changu kikijiinua, waniwinda kama simba; Tena wajionyesha kwangu kuwa wa ajabu. |
17. | Wewe warejeza upya hao mashahidi yako juu yangu, Na kasirani yako waiongeza juu yangu; Jeshi kwa jeshi juu yangu. |
18. | Kwa nini basi kunitoa tumboni? Ningekata roho, lisinione jicho lo lote. |
19. | Ningalikuwa kama mtu asiyekuwapo; Ningalichukuliwa kaburini kutoka tumboni. |
20. | Je! Siku zangu si chache? Acha basi, Usinisumbue, nipate ngaa kutuzwa moyo kidogo. |
21. | Kabla sijaenda huko ambako sitarudi kutoka huko tena, Ni hiyo nchi ya giza, giza tupu; |
22. | Ni nchi ya giza kuu, kama giza lenyewe lilivyo; Ni nchi ya giza tupu, isiyo na matengezo ya mambo yo yote, Nchi ambayo nuru yake ni kama giza. |
← Job (10/42) → |