← 1Chronicles (8/29) → |
1. | Naye Benyamini akamzaa Bela, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Ashbeli, na wa tatu Ahiramu; |
2. | na wa nne Noha, na wa tano Rafa. |
3. | Na Bela alikuwa na wana; Adari, na Gera, na Abihudi; |
4. | na Abishua, na Naamani, na Ahoa; |
5. | na Gera, na Shufamu, na Huramu. |
6. | Na hawa ndio wana wa Ehudi. (Hao ndio wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Geba; nao wakawachukua mateka mpaka Manahathi; |
7. | na Naamani, na Ahoa, na Gera; aliwachukua mateka). Naye akamzaa Uza, na Ahihudi. |
8. | Na Shaharaimu akazaa watoto katika Bara-Moabu, baada ya kuwafukuza wakeze Hushimu na Baara. |
9. | Akazaliwa na Hodeshi, mkewe; Yobabu, na Sibia, na Mesha, na Malkamu; |
10. | na Yeusi, na Shakia, na Mirma. Hao ndio wanawe, wakuu wa mbari za baba zao. |
11. | Naye alikuwa amezaliwa na Hushimu, Abitubu, na Elpaali. |
12. | Na wana wa Elpaali; Eberi, na Mishamu, na Shemedi, ambaye ndiye aliyejenga Ono na Lodi, pamoja na vijiji vyake; |
13. | na Beria, na Shema, waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Aiyaloni, wale ambao waliwakimbiza wenyeji wa Gathi. |
14. | Na Ahio, na Ghashaki, na Yeremothi; |
15. | na Zebadia, na Aradi, na Ederi; |
16. | na Mikaeli, na Ishpa, na Yoha; walikuwa wana wa Beria. |
17. | Na Zebadia, na Meshulamu, na Hizki, na Heberi; |
18. | na Ishmerai, na Izlia, na Yobabu; walikuwa wana wa Elpaali. |
19. | Na Yakimu, na Zikri, na Zabdi; |
20. | na Elienai, na Silethai, na Elieli; |
21. | na Adaya, na Beraya, na Shimrathi; walikuwa wana wa Shema. |
22. | Na Ishpani, na Eberi, na Elieli; |
23. | na Abdoni, na Zikri, na Hanani; |
24. | na Hanania, na Elamu, na Anthothiya; |
25. | na Ifdeya, na Penueli; walikuwa wana wa Shashaki. |
26. | Na Shamsherai, na Sheharia, na Athalia; |
27. | na Yaareshia, na Eliya, na Zikri; walikuwa wana wa Yerohamu. |
28. | Hao ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, katika vizazi vyao vyote, watu maarufu; na hao walikuwa wakikaa Yerusalemu. |
29. | Basi huko Gibea alikaa babaye Gibea, jina lake Yeieli, ambaye jina la mkewe aliitwa Maaka; |
30. | na mwanawe, mzaliwa wake wa kwanza, alikuwa Abdoni, na Suri, na Kishi, na Baali, |
31. | na Gedori, na Ahio, na Zekaria |
32. | Na Miklothi akamzaa Shimea. Na hao nao walikuwa wakikaa pamoja na ndugu zao huko Yerusalemu, kuwakabili ndugu zao. |
33. | Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali. |
34. | Na mwanawe Yonathani alikuwa Meribaali; na Meribaali akamzaa Mika. |
35. | Na wana wa Mika; Pithoni, na Meleki, na Tarea, na Ahazi. |
36. | Na Ahazi akamzaa Yara; na Yara akamzaa Alemethi, na Azmawethi, na Zimri; na Zimri akamzaa Mosa; |
37. | na Mosa akamzaa Binea; na mwanawe huyo alikuwa Refaya, na mwanawe huyo ni Ekasa, na mwanawe huyo ni Aseli; |
38. | naye Aseli alikuwa na wana sita, ambao majina yao ni haya; Azrikamu, na Bokeru, na Ishmaeli, na Shearia, na Obadia, na Hanani. Hao wote walikuwa wana wa Aseli. |
39. | Na wana wa Esheki nduguye ni hawa; mzaliwa wake wa kwanza, Ulamu, na wa pili Yeushi, na wa tatu Elifeleti. |
40. | Na wana wa Ulamu walikuwa watu hodari wa vita, wapiga upinde, nao walikuwa na wana wengi, na wana wa wana, watu mia na hamsini. Hao wote ndio waliokuwa wana wa Benyamini. |
← 1Chronicles (8/29) → |