← 1Chronicles (24/29) → |
1. | Na zamu za wana wa Haruni ni hizi. Wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. |
2. | Lakini hao Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, wala hawakuwa na watoto; kwa hiyo Eleazari na Ithamari wakafanya ukuhani. |
3. | Akawagawanya Daudi, na Sadoki wa wana wa Eleazari, na Ahimeleki wa wana wa Ithamari, katika utumishi kwa kadiri ya usimamizi wao. |
4. | Wakaonekana wakuu wengi wa wana wa Eleazari kuliko wa wana wa Ithamari; wakagawanyika hivi; wa wana wa Eleazari kulikuwa na kumi na sita, waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao; na wa wana wa Ithamari, sawasawa na mbari za baba zao, wanane. |
5. | Ndivyo walivyogawanyika kwa kura, wao kwa wao; kwani kulikuwa na wakuu wa patakatifu, na wakuu wa Mungu, wa wana wa Eleazari, na wa wana wa Ithamari pia. |
6. | Naye Shemaya, mwana wa Nethaneli, mwandishi, aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme, na mbele ya wakuu, na Sadoki kuhani, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari, na wakuu wa mbari za baba za makuhani, na za Walawi; ikatwaliwa ya Eleazari mbari moja ya baba, na moja ikatwaliwa ya Ithamari. |
7. | Kura ya kwanza ikamtokea Yehoiaribu, na ya pili Yedaya; |
8. | ya tatu Harimu, ya nne Seorimu; |
9. | ya tano Malkia, ya sita Miyamini; |
10. | ya saba Hakosi, ya nane Abia; |
11. | ya kenda Yeshua, ya kumi Shekania; |
12. | ya kumi na moja Eliashibu, ya kumi na mbili Yakimu; |
13. | ya kumi na tatu Hupa, ya kumi na nne Yeshebeabu; |
14. | ya kumi na tano Bilga, ya kumi na sita Imeri; |
15. | ya kumi na saba Heziri, ya kumi na nane Hapisesi; |
16. | ya kumi na kenda Pethahia, ya ishirini Ezekieli; |
17. | ya ishirini na moja Yakini, ya ishirini na mbili Gamuli; |
18. | ya ishirini na tatu Delaya, ya ishirini na nne Maazia. |
19. | Huu ndio usimamizi wao katika huduma yao, waingie nyumbani mwa Bwana kwa kadiri ya agizo lao, kwa mkono wa Haruni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyomwamuru. |
20. | Na wa wana wa Lawi, waliosalia; wa wana wa Amramu, Shebueli; wa wana wa Shebueli, Yedeya. |
21. | Wa Rehabia; wa wana wa Rehabia, Ishia mkuu wao. |
22. | Wa Waishari, Shelomothi; wa wana wa Shelomothi, Yahathi. |
23. | Na wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, Yekameamu wa nne. |
24. | Wana wa Uzieli, Mika; wa wana wa Mika, Shamiri. |
25. | Nduguye Mika, Ishia; wa wana wa Ishia, Zekaria. |
26. | Wana wa Merari; Mali na Mushi; wana wa Yaazia; Beno. |
27. | Wana wa Merari; wa Yaazia; Beno, na Shohamu, na Zakuri, na Ibri. |
28. | Wa Mali; Eleazari, asiyekuwa na wana. |
29. | Wa Kishi; wana wa Kishi; Yerameeli. |
30. | Na wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi. Hao ndio wana wa Walawi, kwa kufuata mbari za baba zao. |
31. | Hao nao wakatupiwa kura vile vile, kama ndugu zao wana wa Haruni, machoni pa Daudi mfalme, na Sadoki, na Ahimeleki, na wakuu wa mbari za baba za makuhani na za Walawi; mbari za baba za mkuu, vile vile kama za nduguye mdogo. |
← 1Chronicles (24/29) → |