← 1Chronicles (2/29) → |
1. | Hawa ndio wana wa Israeli; Reubeni, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni; |
2. | na Dani, na Yusufu, na Benyamini, na Naftali, na Gadi, na Asheri. |
3. | Wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela; ambao hao watatu alizaliwa na binti Shua, Mkanaani. Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa Bwana; naye akamwua. |
4. | Na Tamari, mkwewe, akamzalia Peresi, na Zera. Wana wote wa Yuda ni watano. |
5. | Wana wa Peresi; Hesroni, na Hamuli. |
6. | Na wana wa Zera; Zabdi, na Ethani, na Hemani, na Kalkoli, na Darda; hao wote ni watano. |
7. | Na wana wa Karmi; Akani, yule mwenye kutaabisha Israeli, aliyekosa katika kitu kilichowekwa wakfu. |
8. | Na wana wa Ethani; Azaria. |
9. | Tena wana wa Hesroni aliozaliwa; Yerameeli, na Ramu, na Kalebu. |
10. | Na Ramu akamzaa Aminadabu; na Aminadabu akamzaa Nashoni, mkuu wa wana wa Yuda; |
11. | na Nashoni akamzaa Salmoni; na Salmoni akamzaa Boazi; |
12. | na Boazi akamzaa Obedi; na Obedi akamzaa Yese; |
13. | na Yese akamzaa Eliabu, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Abinadabu, na wa tatu Shama; |
14. | na wa nne Nethaneli, na wa tano Radai; |
15. | na wa sita Ozemu, na wa saba Daudi; |
16. | na maumbu yao ni Seruya, na Abigaili. Na wana wa Seruya walikuwa, Abishai, na Yoabu, na Asaheli; hao watatu. |
17. | Na Abigaili akamzaa Amasa; na babaye Amasa ni Yetheri, Mwishmaeli. |
18. | Basi Kalebu, mwana wa Hesroni, akazaliwa wana na mkewe Azubu, na Yeriothi, na hawa ndio wanawe wa kiume; Yesheri, na Shobabu, na Ardoni. |
19. | Akafa Azuba, naye Kalebu akamtwaa Efrathi, aliyemzalia Huri. |
20. | Naye Huri akamzaa Uri; na Uri akamzaa Besaleli. |
21. | Na baadaye Hesroni akamwingilia binti wa Makiri, babaye Gileadi; ambaye alimtwaa alipokuwa mwenye miaka sitini; naye akamzalia Segubu. |
22. | Na Segubu akamzaa Yairi, aliyekuwa mwenye miji ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi. |
23. | Na Geshuri na Aramu wakawapokonya miji ya Yairi, pamoja na Kenathi na miji yake, jumla yote miji sitini. Hao wote ni wana wa Makiri, babaye Gileadi. |
24. | Tena, baada ya kufa kwake Hesroni huko Kalebu-Efrata, ndipo Abia, mkewe Hesroni, alipomzalia Ashuri, babaye Teboa. |
25. | Na wana wa Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, walikuwa Ramu, mzaliwa wa kwanza, na Buna, na Oreni, na Ozemu; kwa Ahiya. |
26. | Naye Yerameeli alikuwa na mke mwingine, jina lake Atara; yeye alikuwa mamaye Onamu. |
27. | Na wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, na Yamini, na Ekeri. |
28. | Na wana wa Onamu walikuwa Shamai, na Yada; na wana wa Shamai; Nadabu, na Abishuri. |
29. | Na mkewe Abishuri aliitwa jina lake Abihaili; naye akamzalia Abani, na Molidi. |
30. | Na wana wa Nadabu; Seledi, na Apaimu; walakini Seledi alikufa hana watoto. |
31. | Na wana wa Apaimu; Ishi. Na wana wa Ishi; Sheshani. Na wana wa Sheshani; Alai. |
32. | Na wana wa Yada, nduguye Shamai; Yetheri, na Yonathani; naye Yetheri akafa hana watoto. |
33. | Na wana wa Yonathani; Pelethi, na Zaza. Hao ndio wana wa Yerameeli. |
34. | Basi huyo Sheshani alikuwa hana wana wa kiume, ila binti. Naye Sheshani alikuwa na mtumwa, Mmisri, jina lake akiitwa Yarha. |
35. | Basi akamwoza binti yake aolewe na Yarha, mtumwa wake; naye akamzalia Atai. |
36. | Na Atai akamzaa Nathani; na Nathani akamzaa Zabadi; |
37. | na Zabadi akamzaa Eflali; na Eflali akamzaa Obedi; |
38. | na Obedi akamzaa Yehu; na Yehu akamzaa Azaria; |
39. | na Azaria akamzaa Helesi; na Helesi akamzaa Eleasa |
40. | na Eleasa akamzaa Sismai; na Sismai akamzaa Shalumu; |
41. | na Shalumu akamzaa Yekamia; na Yekamia akamzaa Elishama. |
42. | Na wana wa Kalebu, nduguye Yerameeli, walikuwa Mesha, mzaliwa wake wa kwanza, aliyekuwa babaye Zifu; na wana wa Maresha, babaye Hebroni. |
43. | Na wana wa Hebroni; Kora, na Tapua, na Rekemu, na Shema. |
44. | Naye Shema akamzaa Rahamu, babaye Yorkeamu; na Rekemu akamzaa Shamai. |
45. | Na mwana wake Shamai alikuwa Maoni; na Maoni alikuwa babaye Bethsuri. |
46. | Naye Efa, suria yake Kalebu, alimzaa Harani, na Mosa, na Gazezi; naye Harani akamzaa Gazezi. |
47. | Na wana wa Yadai; Regemu, na Yothamu, na Geshani, na Peleti, na Efa, na Shaafu. |
48. | Naye Maaka, suria yake Kalebu, akamzalia Sheberi, na Tirhana. |
49. | Tena akamzaa Shaafu, babaye Madmana; na Sheva babaye Makbena; na babaye Gibea; naye binti Kalebu alikuwa Aksa. |
50. | Hao walikuwa wana wa Kalebu. Wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi; Shobali, babaye Kiriath-Yearimu; |
51. | Salma, babaye Bethlehemu; na Harefu, babaye Beth-gaderi. |
52. | Naye Shobali, babaye Kiriath-Yearimu, alikuwa na wana; Haroe, na nusu ya Wamenuhothi. |
53. | Na jamaa za Kiriath-Yearimu; Waithri, na Waputhi, na Washumathi, na Wamishrai; katika hao walitoka Wasorathi, na Waeshtaoli. |
54. | Na wana wa Salma; Bethlehemu, na Wanetofathi, Atroth-beth-Yoabu, na nusu ya Wamenuhothi, na Wazori. |
55. | Na jamaa za waandishi waliokaa Yabesi; Watirathi, na Washimeathi, na Wasukathi. Hao ndio Wakeni, waliotoka kwake Hamathi, babaye mbari ya Rekabu. |
← 1Chronicles (2/29) → |