← 1Chronicles (16/29) → |
1. | Wakaliingiza sanduku la Mungu, na kuliweka katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake; wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu. |
2. | Na Daudi alipokwisha kuitoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Bwana. |
3. | Kisha akawagawia kila mtu wa Israeli, waume kwa wake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu. |
4. | Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la Bwana, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, Bwana, Mungu wa Israeli; |
5. | Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Matithiya, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi; |
6. | nao makuhani Benaya na Yahazieli wenye baragumu daima, mbele ya sanduku la agano la Mungu. |
7. | Ndipo siku hiyo Daudi alipoagiza kwanza kumshukuru Bwana, kwa mkono wa Asafu na nduguze. |
8. | Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; Wajulisheni watu matendo yake. |
9. | Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi; Zitafakarini ajabu zake zote. |
10. | Jisifuni kwa jina lake takatifu; Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana. |
11. | Mtakeni Bwana na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote. |
12. | Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya; Miujiza yake na hukumu za kinywa chake; |
13. | Enyi wazao wa Israeli, mtumishi wake, Enyi wana wa Yakobo, wateule wake. |
14. | Yeye, Bwana, ndiye Mungu wetu; Duniani mwote mna hukumu zake. |
15. | Likumbukeni agano lake milele, Neno lile aliloviamuru vizazi elfu. |
16. | Agano alilofanya na Ibrahimu, Na uapo wake kwa Isaka; |
17. | Alilomthibitishia Yakobo kuwa amri, Na Israeli liwe agano la milele. |
18. | Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani, Iwe urithi wenu mliopimiwa; |
19. | Mlipokuwa watu wawezao kuhesabiwa; Naam, watu wachache na wageni ndani yake. |
20. | Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa, Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine. |
21. | Hakumwacha mtu awaonee; Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao; |
22. | Akisema, Msiwaguse masihi |
23. | Mwimbieni Bwana, nchi yote; Tangazeni wokovu wake siku kwa siku. |
24. | Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake. |
25. | Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana; Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote. |
26. | Maana miungu yote ya watu si kitu; Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu. |
27. | Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake. |
28. | Mpeni Bwana, enyi jamaa za watu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu. |
29. | Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu; |
30. | Tetemekeni mbele zake, nchi yote. |
31. | Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie; Na waseme katika mataifa, Bwana ametamalaki; |
32. | Bahari na ivume na vyote viijazavyo; Mashamba na yashangilie na vyote vilivyomo; |
33. | Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha, |
34. | Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
35. | Nanyi mkaseme, Ee Mungu wa wokovu wetu, utuokoe, Utukusanye kwa kututoa katika mataifa, Tulishukuru jina lako takatifu, Tuzifanyie shangwe sifa zako. |
36. | Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele hata milele. Na watu wote wakasema, Amina; wakamhimidi Bwana. |
37. | Basi akawaacha huko, mbele ya sanduku la agano la Bwana, Asafu na nduguze, ili watumike mbele ya sanduku daima, kila siku kama ilivyokuwa kazi yake. |
38. | Naye Obed-edomu, pamoja na ndugu zao, sitini na wanane; Obed-edomu na mwana wa Yeduthuni, na Hosa, wawe mabawabu; |
39. | na Sadoki kuhani, na nduguze makuhani, mbele ya maskani ya Bwana katika mahali pa juu palipokuwa huko Gibeoni, |
40. | ili kumtolea Bwana sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa daima asubuhi na jioni, naam, sawasawa na yote yaliyoandikwa katika torati ya Bwana, aliyowaamuru Israeli; |
41. | na pamoja nao Hemani na Yeduthuni, na wale wengine waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru Bwana, kwa kuwa fadhili zake ni za milele; |
42. | na pamoja nao Hemani na Yeduthuni wenye baragumu na matoazi, kwa hao watakaovumisha sauti, na vinanda kwa ajili ya hizo nyimbo za Mungu; na hao wana wa Yeduthuni wawepo mlangoni. |
43. | Kisha watu wote wakaenda zao kila mtu nyumbani kwake; naye Daudi akarudi ili awabariki watu wa nyumbani mwake. |
← 1Chronicles (16/29) → |