Psalms (99/150)  

1. Bwana ametamalaki, mataifa wanatetemeka; Ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika.
2. Bwana katika Sayuni ni mkuu, Naye ametukuka juu ya mataifa yote.
3. Na walishukuru jina lake kuu la kuhofiwa; Ndiye mtakatifu.
4. Nguvu za mfalme nazo zapenda hukumu; Wewe ndiwe uliyeithibitisha adili; Ulifanya hukumu na haki katika Yakobo.
5. Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu; Sujuduni penye kiti cha miguu yake; Ndiye mtakatifu.
6. Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake, Na Samweli miongoni mwao waliitiao jina lake, Walipomwita Bwana aliwaitikia;
7. Katika nguzo ya wingu alikuwa akisema nao. Walishika shuhuda zake na amri aliyowapa.
8. Ee Bwana, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu; Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe Ingawa uliwapatiliza matendo yao.
9. Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu; Maana Bwana, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.

  Psalms (99/150)