Psalms (98/150)  

1. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.
2. Bwana ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.
3. Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu.
4. Mshangilieni Bwana, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.
5. Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi.
6. Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, Bwana.
7. Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake.
8. Mito na ipige makofi, Milima na iimbe pamoja kwa furaha.
9. Mbele za Bwana; Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa adili.

  Psalms (98/150)