| ← Psalms (93/150) → |
| 1. | Bwana ametamalaki, amejivika adhama, Bwana amejivika, na kujikaza nguvu. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike; |
| 2. | Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani; Wewe ndiwe uliye tangu milele. |
| 3. | Ee Bwana, mito imepaza, Mito imepaza sauti zake, Mito imepaza uvumi wake. |
| 4. | Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu, Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo, Bwana Aliye juu ndiye mwenye ukuu. |
| 5. | Shuhuda zako ni amini sana; Utakatifu ndio uifaao nyumba yako, Ee Bwana, milele na milele. |
| ← Psalms (93/150) → |