| ← Psalms (92/150) → |
| 1. | Ni neno jema kumshukuru Bwana, Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu. |
| 2. | Kuzitangaza rehema zako asubuhi, Na uaminifu wako wakati wa usiku. |
| 3. | Kwa chombo chenye nyuzi kumi, Na kwa kinanda, Na kwa mlio wa kinubi. |
| 4. | Kwa kuwa umenifurahisha, Bwana, Kwa kazi yako; nitashangilia Kwa ajili ya matendo ya mikono yako. |
| 5. | Ee Bwana, jinsi yalivyo makuu matendo yako! Mawazo yako ni mafumbo makubwa. |
| 6. | Mtu mjinga hayatambui hayo, Wala mpumbavu hayafahamu. |
| 7. | Wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakistawi. Ni kwa kusudi waangamizwe milele; |
| 8. | Bali Wewe, Bwana, U Mtukufu hata milele. |
| 9. | Maana hao adui zako, Ee Bwana, Hao adui zako watapotea, Na watendao maovu watatawanyika wote pia. |
| 10. | Bali pembe yangu umeiinua kama pembe ya nyati, Nimepakwa mafuta mabichi. |
| 11. | Na jicho langu limewatazama walioniotea, Sikio langu limesikia habari za waovu walionishambulia. |
| 12. | Mwenye haki atasitawi kama mtende, Atakua kama mwerezi wa Lebanoni. |
| 13. | Waliopandwa katika nyumba ya Bwana Watasitawi katika nyua za Mungu wetu. |
| 14. | Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi. |
| 15. | Watangaze ya kuwa Bwana ni mwenye adili, Mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu. |
| ← Psalms (92/150) → |