| ← Psalms (9/150) → |
| 1. | Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu; |
| 2. | Nitafurahi na kukushangilia Wewe; Nitaliimbia jina lako, Wewe Uliye juu. |
| 3. | Kwa sababu adui zangu hurudi nyuma; Hujikwaa na kuangamia mbele zako. |
| 4. | Kwa maana umenifanyia hukumu na haki Umeketi kitini pa enzi ukihukumu kwa haki. |
| 5. | Umewakemea mataifa; Na kumwangamiza mdhalimu; Umelifuta jina lao milele na milele; |
| 6. | Adui wamekoma na kuachwa ukiwa milele. Nayo miji yao uliing'oa; Hata kumbukumbu lao limepotea. |
| 7. | Bali Bwana atakaa milele, Ameweka kiti chake tayari kwa hukumu. |
| 8. | Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki; Atawaamua watu kwa adili. |
| 9. | Bwana atakuwa ngome kwake aliyeonewa, Naam, ngome kwa nyakati za shida. |
| 10. | Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe, Maana Wewe, Bwana hukuwaacha wakutafutao. |
| 11. | Mwimbieni Bwana akaaye Sayuni, Yatangazeni kati ya watu matendo yake. |
| 12. | Maana mlipiza kisasi cha damu awakumbuka, Hakukisahau kilio cha wanyonge. |
| 13. | Wewe, Bwana, unifadhili, Tazama mateso niteswayo na wanaonichukia; Wewe uniinuaye katika malango ya mauti, |
| 14. | Ili nizisimulie sifa zako zote; Katika malango ya binti Sayuni Nitaufurahia wokovu wako. |
| 15. | Mataifa wamezama katika shimo walilolifanya; Kwa wavu waliouficha imenaswa miguu yao. |
| 16. | Bwana amejidhihirisha na kutekeleza hukumu; Amemnasa mdhalimu kwa kazi ya mikono yake. |
| 17. | Wadhalimu watarejea kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu. |
| 18. | Kwa maana mhitaji hatasahauliwa daima; Matumaini ya wanyonge hayatapotea milele. |
| 19. | Bwana, usimame, mwanadamu asipate nguvu, Mataifa wahukumiwe mbele zako. |
| 20. | Bwana, uwawekee kitisho, Mataifa na wajijue kuwa ni binadamu. |
| ← Psalms (9/150) → |