Psalms (87/150)  

1. Msingi wake upo Juu ya milima mitakatifu.
2. Bwana ayapenda malango ya Sayuni Kuliko maskani zote za Yakobo.
3. Umetajwa kwa mambo matukufu, Ee Mji wa Mungu.
4. Nitataja Rahabu na Babeli Miongoni mwao wanaonijua. Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi; Huyu alizaliwa humo.
5. Naam, mintarafu Sayuni itasemwa, Huyu na huyu alizaliwa humo. Na Yeye Aliye juu Ataufanya imara.
6. Bwana atahesabu, awaandikapo mataifa, Huyu alizaliwa humo.
7. Waimbao na wachezao na waseme, Visima vyangu vyote vimo mwako.

  Psalms (87/150)