| ← Psalms (84/150) → |
| 1. | Maskani zako zapendeza kama nini, Ee Bwana wa majeshi! |
| 2. | Nafsi yangu imezionea shauku nyua za Bwana, Naam, na kuzikondea. Moyo wangu na mwili wangu Vinamlilia Mungu aliye hai. |
| 3. | Shomoro naye ameona nyumba, Na mbayuwayu amejipatia kioto, Alipoweka makinda yake, Kwenye madhabahu zako, Ee Bwana wa majeshi, Mfalme wangu na Mungu wangu. |
| 4. | Heri wakaao nyumbani mwako, Wanakuhimidi daima. |
| 5. | Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako, Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake. |
| 6. | Wakipita kati ya bonde la Vilio, Hulifanya kuwa chemchemi, Naam, mvua ya vuli hulivika baraka |
| 7. | Huendelea toka nguvu hata nguvu, Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu. |
| 8. | Bwana, Mungu wa majeshi, uyasikie maombi yangu, Ee Mungu wa Yakobo, usikilize, |
| 9. | Ee Mungu, ngao yetu, uangalie, Umtazame uso masihi |
| 10. | Hakika siku moja katika nyua zako Ni bora kuliko siku elfu. Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kukaa katika hema za uovu. |
| 11. | Kwa kuwa Bwana, Mungu, ni jua na ngao, Bwana atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu. |
| 12. | Ee Bwana wa majeshi, Heri mwanadamu anayekutumaini Wewe. |
| ← Psalms (84/150) → |