← Psalms (83/150) → |
1. | Ee Mungu, usistarehe, Ee Mungu, usinyamae, wala usitulie. |
2. | Maana adui zako wanafanya ghasia, Nao wakuchukiao wameviinua vichwa vyao. |
3. | Juu ya watu wako wanafanya hila, Na kushauriana juu yao uliowaficha. |
4. | Wamesema, Njoni, tuwakatilie mbali wasiwe taifa, Na jina la Israeli halitakumbukwa tena. |
5. | Maana wanashauriana kwa moyo mmoja, Juu yako wanafanyana agano. |
6. | Hema za Edomu, na Waishmaeli, Na Moabu, na Wahagari, |
7. | Gebali, na Amoni, na Amaleki, Na Filisti, nao wanaokaa Tiro, |
8. | Ashuri naye amepatana nao, Wamewasaidia wana wa Lutu. |
9. | Uwatende kama Midiani, kama Sisera, Kama Yabini, penye kijito Kishoni. |
10. | Ambao waliangamizwa Endori; Wakawa samadi juu ya nchi. |
11. | Uwafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu, Na masheki yao wote kama Zeba na Zalmuna. |
12. | Ambao Walisema, Na tutamalaki makao ya Mungu. |
13. | Ee Mungu, uwafanye kama mavumbi ya kisulisuli, Mithili ya makapi mbele ya upepo, |
14. | Kama moto uteketezao msitu, Kama miali ya moto iiwashayo milima, |
15. | Ndivyo utakavyowafuatia kwa tufani yako, Na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako. |
16. | Uwajaze nyuso zao fedheha; Wakalitafute jina lako, Bwana. |
17. | Waaibike, wafadhaike milele, Naam, watahayarike na kupotea. |
18. | Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote. |
← Psalms (83/150) → |