Psalms (82/150)  

1. Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu; Katikati ya miungu anahukumu.
2. Hata lini mtahukumu kwa dhuluma, Na kuzikubali nyuso za wabaya?
3. Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa na fukara;
4. Mwokoeni maskini na mhitaji; Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.
5. Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; Misingi yote ya nchi imetikisika.
6. Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia.
7. Lakini mtakufa kama wanadamu, Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.
8. Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi, Maana Wewe utawarithi mataifa yote.

  Psalms (82/150)