| ← Psalms (81/150) → |
| 1. | Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha, Mshangilieni Mungu wa Yakobo. |
| 2. | Pazeni zaburi, pigeni matari, Kinubi chenye sauti nzuri, na kinanda. |
| 3. | Pigeni panda mwandamo wa mwezi, Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu. |
| 4. | Kwa maana ni sheria kwa Israeli, Ni hukumu ya Mungu wa Yakobo. |
| 5. | Aliamuru iwe ushuhuda katika Yusufu, Alipoondoka juu ya nchi ya Misri; Maneno yake nisiyemjua naliyasikia. |
| 6. | Nimelitenga bega lake na mzigo, Mikono yake ikaachana na kikapu. |
| 7. | Katika shida uliniita nikakuokoa; Nalikuitikia katika sitara ya radi; Nalikujaribu penye maji ya Meriba. |
| 8. | Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya, Ee Israeli, kama ukitaka kunisikiliza; |
| 9. | Usiwe na mungu mgeni ndani yako; Wala usimsujudie mungu mwingine. |
| 10. | Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, Niliyekupandisha toka nchi ya Misri; Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza. |
| 11. | Lakini watu wangu hawakuisikiliza sauti yangu, Wala Israeli hawakunitaka. |
| 12. | Nikawaacha wakaenda kwa ukaidi wa mioyo yao, Waenende katika mashauri yao. |
| 13. | Laiti watu wangu wangenisikiliza, Na Israeli angeenenda katika njia zangu; |
| 14. | Ningewadhili adui zao kwa upesi, Na juu ya watesi wao ningegeuza mkono wangu; |
| 15. | Wamchukiao Bwana wangenyenyekea mbele zake, Bali wakati wao ungedumu milele. |
| 16. | Naam, ningewalisha kwa unono wa ngano, Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani. |
| ← Psalms (81/150) → |