Psalms (70/150)  

1. Ee Mungu, uniokoe, Ee Bwana, unisaidie hima.
2. Waaibike, wafedheheke, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu.
3. Warudi nyuma, na iwe aibu yao, Wanaosema, Ewe! Ewe!
4. Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu.
5. Nami ni maskini na mhitaji, Ee Mungu, unijilie kwa haraka. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Bwana, usikawie.

  Psalms (70/150)