| ← Psalms (61/150) → |
| 1. | Ee Mungu, ukisikie kilio changu, Uyasikilize maombi yangu. |
| 2. | Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda. |
| 3. | Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, Ngome yenye nguvu adui asinipate. |
| 4. | Nitakaa katika hema yako milele, Nitaikimbilia sitara ya mbawa zako |
| 5. | Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu. Umewapa urithi wao waliogopao jina lako. |
| 6. | Utaziongeza siku za mfalme, Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi. |
| 7. | Atakaa mbele za Mungu milele, Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi. |
| 8. | Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima, Ili niondoe nadhiri zangu kila siku. |
| ← Psalms (61/150) → |