← Psalms (60/150) → |
1. | Ee Mungu, umetutupa na kututawanya, Umekuwa na hasira, uturudishe tena. |
2. | Umeitetemesha nchi na kuipasua, Upaponye palipobomoka, maana inatikisika. |
3. | Umewaonyesha watu wako mazito, Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha. |
4. | Umewapa wakuogopao bendera, Ili itwekwe kwa ajili ya kweli. |
5. | Ili wapenzi wako waopolewe, Uokoe kwa mkono wako wa kuume, utuitikie. |
6. | Mungu amenena kwa utakatifu wake, Nami nitashangilia. Nitaigawanya Shekemu, Nitalipima bonde la Sukothi. |
7. | Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu, Na Efraimu ni nguvu ya kichwa changu. Yuda ni fimbo yangu ya kifalme, |
8. | Moabu ni bakuli langu la kunawia. Nitamtupia Edomu kiatu changu, Na kumpigia Filisti kelele za vita. |
9. | Ni nani atakayenipeleka hata mji wenye boma? Ni nani atakayeniongoza hata Edomu? |
10. | Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa? Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu? |
11. | Utuletee msaada juu ya mtesi, Maana wokovu wa binadamu haufai. |
12. | Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu. |
← Psalms (60/150) → |