Psalms (6/150)  

1. Bwana, usinikemee kwa hasira yako, Wala usinirudi kwa ghadhabu yako.
2. Bwana, unifadhili, maana ninanyauka; Bwana, uniponye, mifupa yangu imefadhaika.
3. Na nafsi yangu imefadhaika sana; Na Wewe, Bwana, hata lini?
4. Bwana urudi, uniopoe nafsi yangu, Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
5. Maana mautini hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?
6. Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakieleza kitanda changu; Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu.
7. Jicho langu limeharibika kwa masumbufu, Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi.
8. Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu; Kwa kuwa Bwana ameisikia sauti ya kilio changu.
9. Bwana ameisikia dua yangu; Bwana atayatakabali maombi yangu.
10. Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, Watarudi nyuma, kwa ghafula wataaibika.

  Psalms (6/150)