← Psalms (59/150) → |
1. | Ee Mungu wangu, uniponye na adui zangu, Uniinue juu yao wanaoshindana nami. |
2. | Uniponye nao wafanyao maovu, Uniokoe na watu wa damu. |
3. | Kwa maana wanaiotea nafsi yangu; Wenye nguvu wamenikusanyikia; Ee Bwana, si kwa kosa langu, Wala si kwa hatia yangu. |
4. | Bila kosa langu huenda mbio, hujiweka tayari; Uamke uonane nami, na kutazama. |
5. | Na Wewe, Bwana, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, uamke. Uwapatilize mataifa yote; Usiwarehemu waovu wafanyao uovu hata mmoja. |
6. | Wakati wa jioni hurudi, hulia kama mbwa, Na kuzunguka-zunguka mjini. |
7. | Tazama, kwa vinywa vyao huteuka, Midomoni mwao mna panga, Kwa maana ni nani asikiaye? |
8. | Na Wewe, Bwana, utawacheka, Utawadhihaki mataifa yote. |
9. | Ee nguvu zangu, nitakungoja Wewe, Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu |
10. | Mungu wa fadhili zangu atanitangulia, Mungu atanijalia kuwatazama adui zangu. |
11. | Usiwaue, watu wangu wasije wakasahau; Uwatawanye kwa uweza wako, Na kuwaangamiza, Ee Bwana, ngao yetu. |
12. | Kwa dhambi ya kinywa chao, Na kwa neno la midomo yao, Wanaswe kwa kiburi chao, Kwa ajili ya kulaani na uongo wasemao. |
13. | Uwakomeshe kwa hasira, Uwakomeshe watoweke, Wajue ya kuwa Mungu atawala katika Yakobo, Na hata miisho ya dunia. |
14. | Wakati wa jioni hurudi, hulia kama mbwa, Na kuzunguka-zunguka mjini. |
15. | Watatanga-tanga hao wakitafuta chakula; Wasiposhiba watakesha usiku kucha. |
16. | Nami nitaziimba nguvu zako asubuhi, Nitaziimba fadhili zako kwa furaha. Kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu, Na makimbilio siku ya shida yangu. |
17. | Ee nguvu zangu, nitakuimbia kwa furaha, Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu, Mungu wa fadhili zangu. |
← Psalms (59/150) → |