← Psalms (57/150) → |
1. | Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi, Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe. Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako, Hata misiba hii itakapopita. |
2. | Nitamwita MUNGU Aliye juu, Mungu anitimiziaye mambo yangu. |
3. | Atapeleka toka mbinguni na kuniokoa, Atukanapo yule atakaye kunimeza. Mungu atazipeleka Fadhili zake na kweli yake |
4. | Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali. |
5. | Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako. |
6. | Wameweka wavu ili kuninasa miguu; Nafsi yangu imeinama; Wamechimba shimo mbele yangu; Wametumbukia ndani yake! |
7. | Ee Mungu, moyo wangu u thabiti, Moyo wangu u thabiti. Nitaimba, nitaimba zaburi, |
8. | Amka, utukufu wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri. |
9. | Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu, Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa. |
10. | Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni, Na uaminifu wako hata mawinguni. |
11. | Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako. |
← Psalms (57/150) → |