Psalms (54/150)  

1. Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe, Na kwa uweza wako unifanyie hukumu.
2. Ee Mungu, uyasikie maombi yangu, Uyasikilize maneno ya kinywa changu.
3. Kwa maana wageni wamenishambulia; Watu watishao wananitafuta nafsi yangu; Hawakumweka Mungu mbele yao.
4. Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia; Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu.
5. Atawarudishia adui zangu ubaya wao; Uwaangamize kwa uaminifu wako.
6. Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu; Ee Bwana, nitalishukuru jina lako, maana ni jema.
7. Kwa kuwa limeniokoa na kila taabu; Na jicho langu limeridhika Kwa kuwatazama adui zangu.

  Psalms (54/150)