Psalms (52/150)  

1. Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote.
2. Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila
3. Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli.
4. Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila.
5. Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung'oa katika nchi ya walio hai.
6. Nao wenye haki wataona; Wataingiwa na hofu na kumcheka;
7. Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kujifanya hodari kwa madhara yake.
8. Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.
9. Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako.

  Psalms (52/150)