← Psalms (5/150) → |
1. | Ee Bwana, uyasikilize maneno yangu, Ukuangalie kutafakari kwangu. |
2. | Uisikie sauti ya kilio changu, Ee Mfalme wangu na Mungu wangu, Kwa maana Wewe ndiwe nikuombaye. |
3. | Bwana, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia. |
4. | Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya; Mtu mwovu hatakaa kwako; |
5. | Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako; Unawachukia wote watendao ubatili. |
6. | Utawaharibu wasemao uongo; Bwana humzira mwuaji na mwenye hila |
7. | Bali mimi, kwa wingi wa fadhili zako, Nitaingia nyumbani mwako; Na kusujudu kwa kicho, Nikilielekea hekalu lako takatifu. |
8. | Bwana, uniongoze kwa haki yako, Kwa sababu yao wanaoniotea. Uisawazishe njia yako mbele ya uso wangu, |
9. | Maana vinywani mwao hamna uaminifu; Mtima wao ni shimo tupu, koo lao ni kaburi wazi, Ulimi wao hujipendekeza. |
10. | Wewe, Mungu, uwapatilize, Na waanguke kwa mashauri yao. Uwatoe nje kwa ajili ya wingi wa makosa yao, Kwa maana wamekuasi Wewe. |
11. | Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia. |
12. | Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki; Bwana, utamzungushia radhi kama ngao. |
← Psalms (5/150) → |