← Psalms (48/150) → |
1. | Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu. |
2. | Kuinuka kwake ni mzuri sana, Ni furaha ya dunia yote. Mlima Sayuni pande za kaskazini, Mji wa Mfalme mkuu. |
3. | Mungu katika majumba yake Amejijulisha kuwa ngome. |
4. | Maana, tazama, wafalme walikusanyika; Walipita wote pamoja. |
5. | Waliona, mara wakashangaa; Wakafadhaika na kukimbia. |
6. | Papo hapo tetemeko liliwashika, Utungu kama wa mwanamke azaaye. |
7. | Kwa upepo wa mashariki Wavunja jahazi za Tarshishi. |
8. | Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona, Katika mji wa Bwana wa majeshi. Mji wa Mungu wetu; Mungu ataufanya imara hata milele. |
9. | Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu, Katikati ya hekalu lako. |
10. | Kama lilivyo jina lako, Ee Mungu, Ndivyo na sifa yako hata miisho ya dunia. Mkono wako wa kuume umejaa haki; |
11. | Na ufurahi mlima Sayuni. Binti za Yuda na washangilie Kwa sababu ya hukumu zako. |
12. | Tembeeni katika Sayuni, Uzungukeni mji, Ihesabuni minara yake, |
13. | Tieni moyoni boma zake, Yafikirini majumba yake, Mpate kuwaambia kizazi kitakachokuja. |
14. | Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele Yeye ndiye atakayetuongoza. |
← Psalms (48/150) → |