← Psalms (46/150) → |
1. | Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. |
2. | Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. |
3. | Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake. |
4. | Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye juu. |
5. | Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa; Mungu atausaidia asubuhi na mapema. |
6. | Mataifa yalighadhibika, falme zikataharuki; Alitoa sauti yake, nchi ikayeyuka. |
7. | Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. |
8. | Njoni myatazame matendo ya Bwana, Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi. |
9. | Avikomesha vita hata mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari. |
10. | Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi. |
11. | Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. |
← Psalms (46/150) → |