| ← Psalms (41/150) → |
| 1. | Heri amkumbukaye mnyonge; Bwana atamwokoa siku ya taabu. |
| 2. | Bwana atamlinda na kumhifadhi hai, Naye atafanikiwa katika nchi; Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake. |
| 3. | Bwana atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani. Katika ugonjwa wake umemtandikia. |
| 4. | Nami nalisema, Bwana, unifadhili, Uniponye roho yangu maana nimekutenda dhambi. |
| 5. | Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya, Atakufa lini, jina lake likapotea? |
| 6. | Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo, Moyo wake hujikusanyia maovu, Naye atokapo nje huyanena. |
| 7. | Wote wanaonichukia wananinong'ona, Wananiwazia mabaya. |
| 8. | Neno la kisirani limemgandama, Na iwapo amelala hatasimama tena. |
| 9. | Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake. |
| 10. | Lakini Wewe, Bwana, unifadhili, Uniinue nipate kuwalipa. |
| 11. | Kwa neno hili nimejua ya kuwa wapendezwa nami, Kwa kuwa adui yangu hasimangi kwa kunishinda. |
| 12. | Nami katika ukamilifu wangu umenitegemeza, Umeniweka mbele za uso wako milele. |
| 13. | Na atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Tangu milele hata milele. Amina na Amina. |
| ← Psalms (41/150) → |