| ← Psalms (36/150) → |
| 1. | Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake, Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake. |
| 2. | Kwa maana hujipendekeza machoni pake Kuwa upotovu wake hautaonekana na kuchukiwa. |
| 3. | Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila, Ameacha kuwa na akili na kutenda mema. |
| 4. | Huwaza maovu kitandani pake, Hujiweka katika njia mbaya; ubaya hauchukii. |
| 5. | Ee Bwana, fadhili zako zafika hata mbinguni, Uaminifu wako hata mawinguni. |
| 6. | Haki yako ni kama milima ya Mungu, Hukumu zako ni vilindi vikuu, Ee Bwana, unawaokoa wanadamu na wanyama. |
| 7. | Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako! Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako. |
| 8. | Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako, Nawe utawanywesha mto wa furaha zako. |
| 9. | Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima, Katika nuru yako tutaona nuru. |
| 10. | Uwadumishie wakujuao fadhili zako, Na wanyofu wa moyo uaminifu wako. |
| 11. | Mguu wa kiburi usinikaribie, Wala mkono wa wasio haki usinifukuze. |
| 12. | Huko ndiko walikoanguka wafanyao maovu; Wameangushwa chini wasiweze kusimama. |
| ← Psalms (36/150) → |