| ← Psalms (3/150) → |
| 1. | Bwana, watesi wangu wamezidi kuwa wengi, Ni wengi wanaonishambulia, |
| 2. | Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu. |
| 3. | Na Wewe, Bwana, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu. |
| 4. | Kwa sauti yangu namwita Bwana Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. |
| 5. | Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa Bwana ananitegemeza. |
| 6. | Sitayaogopa makumi elfu ya watu, Waliojipanga juu yangu pande zote. |
| 7. | Bwana, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki. |
| 8. | Wokovu una Bwana; Baraka yako na iwe juu ya watu wako. |
| ← Psalms (3/150) → |