| ← Psalms (29/150) → |
| 1. | Mpeni Bwana, enyi wana wa Mungu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu; |
| 2. | Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu. |
| 3. | Sauti ya Bwana i juu ya maji; Mungu wa utukufu alipiga radi; Bwana yu juu ya maji mengi. |
| 4. | Sauti ya Bwana ina nguvu; Sauti ya Bwana ina adhama; |
| 5. | Sauti ya Bwana yaivunja mierezi; Naam, Bwana aivunja-vunja mierezi ya Lebanoni; |
| 6. | Airusha-rusha kama ndama wa ng'ombe; Lebanoni na Sirioni kama mwana-nyati. |
| 7. | Sauti ya Bwana yaipasua miali ya moto; |
| 8. | Sauti ya Bwana yalitetemesha jangwa; Bwana alitetemesha jangwa la Kadeshi. |
| 9. | Sauti ya Bwana yawazalisha ayala, Na kuifichua misitu; Na ndani ya hekalu lake Wanasema wote, Utukufu. |
| 10. | Bwana aliketi juu ya Gharika; Naam, Bwana ameketi hali ya mfalme milele. |
| 11. | Bwana atawapa watu wake nguvu; Bwana atawabariki watu wake kwa amani. |
| ← Psalms (29/150) → |