| ← Psalms (24/150) → |
| 1. | Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake. |
| 2. | Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. |
| 3. | Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? |
| 4. | Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila. |
| 5. | Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake. |
| 6. | Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. |
| 7. | Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. |
| 8. | Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita. |
| 9. | Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. |
| 10. | Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Bwana wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu. |
| ← Psalms (24/150) → |