← Psalms (22/150) → |
1. | Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua kwangu? |
2. | Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu Na wakati wa usiku lakini sipati raha. |
3. | Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli. |
4. | Baba zetu walikutumaini Wewe, Walitumaini, na Wewe ukawaokoa. |
5. | Walikulilia Wewe wakaokoka, Walikutumaini wasiaibike. |
6. | Lakini mimi ni mdudu wala si mtu, Laumu ya wanadamu na mzaha wa watu. |
7. | Wote wanionao hunicheka sana, Hunifyonya, wakitikisa vichwa vyao; |
8. | Husema, Umtegemee Bwana; na amponye; Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye. |
9. | Naam, Wewe ndiwe uliyenitoa tumboni, Ulinitumainisha matitini mwa mama yangu. |
10. | Kwako nalitupwa tangu tumboni, Toka tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu wangu. |
11. | Usiwe mbali nami maana taabu i karibu, Kwa maana hakuna msaidizi. |
12. | Mafahali wengi wamenizunguka, Walio hodari wa Bashani wamenisonga; |
13. | Wananifumbulia vinywa vyao, Kama simba apapuraye na kunguruma. |
14. | Nimemwagika kama maji, Mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya mtima wangu. |
15. | Nguvu zangu zimekauka kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya zangu; Unaniweka katika mavumbi ya mauti |
16. | Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenizua mikono na miguu. |
17. | Naweza kuihesabu mifupa yangu yote; Wao wananitazama na kunikodolea macho. |
18. | Wanagawanya nguo zangu, Na vazi langu wanalipigia kura. |
19. | Nawe, Bwana, usiwe mbali, Ee Nguvu zangu, fanya haraka kunisaidia. |
20. | Uniponye nafsi yangu na upanga, Mpenzi wangu na nguvu za mbwa. |
21. | Kinywani mwa simba uniokoe; Naam, toka pembe za nyati umenijibu. |
22. | Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu, Katikati ya kusanyiko nitakusifu. |
23. | Ninyi mnaomcha Bwana, msifuni, Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo, mtukuzeni, Mcheni, enyi nyote mlio wazao wa Israeli. |
24. | Maana hakulidharau teso la mteswa, Wala hakuchukizwa nalo; Wala hakumficha uso wake, Bali alipomlilia akamsikia. |
25. | Kwako zinatoka sifa zangu Katika kusanyiko kubwa. Nitaziondoa nadhiri zangu Mbele yao wamchao. |
26. | Wapole watakula na kushiba, Wamtafutao Bwana watamsifu; Mioyo yenu na iishi milele. |
27. | Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea Bwana; Jamaa zote za mataifa watamsujudia. |
28. | Maana ufalme una Bwana, Naye ndiye awatawalaye mataifa. |
29. | Wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu, Humwinamia wote washukao mavumbini; Naam, yeye asiyeweza kujihuisha nafsi yake, |
30. | Wazao wake watamtumikia. Zitasimuliwa habari za Bwana, Kwa kizazi kitakachokuja, |
31. | Nao watawahubiri watakaozaliwa haki yake, Ya kwamba ndiye aliyeyafanya. |
← Psalms (22/150) → |