← Psalms (18/150) → |
1. | Wewe, Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana; |
2. | Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu. |
3. | Nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu. |
4. | Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. |
5. | Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya mauti ikanikabili. |
6. | Katika shida yangu nalimwita Bwana, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake. |
7. | Ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka, Misingi ya milima ikasuka-suka; Ikatikisika kwa sababu alikuwa na ghadhabu. |
8. | Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto ukatoka kinywani mwake ukala, Makaa yakawashwa nao. |
9. | Aliziinamisha mbingu akashuka, Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake. |
10. | Akapanda juu ya kerubi akaruka, Naam, aliruka upesi juu ya mabawa ya upepo. |
11. | Alifanya giza kuwa mahali pake pa kujificha, Kuwa hema yake ya kumzunguka. Giza la maji na mawingu makuu ya mbinguni. |
12. | Toka mwangaza uliokuwa mbele zake Kukapita mawingu yake makuu. Mvua ya mawe na makaa ya moto. |
13. | Bwana alipiga radi mbinguni, Yeye Aliye juu akaitoa sauti yake, Mvua ya mawe na makaa ya moto. |
14. | Akaipiga mishale yake akawatawanya, Naam, umeme mwingi sana, akawatapanya. |
15. | Ndipo ilipoonekana mikondo ya maji, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Ee Bwana, kwa kukemea kwako, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwako. |
16. | Alipeleka kutoka juu akanishika, Na kunitoa katika maji mengi. |
17. | Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, Na wale walionichukia, Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi. |
18. | Walinikabili siku ya msiba wangu, Lakini Bwana alikuwa tegemeo langu. |
19. | Akanitoa akanipeleka panapo nafasi, Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami. |
20. | Bwana alinitendea sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa. |
21. | Maana nimezishika njia za Bwana, Wala sikumwasi Mungu wangu. |
22. | Hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu, Wala amri zake sikujiepusha nazo. |
23. | Nami nalikuwa mkamilifu mbele zake, Nikajilinda na uovu wangu. |
24. | Mradi Bwana amenilipa sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake. |
25. | Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili; Kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu; |
26. | Kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu; Na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi. |
27. | Maana Wewe utawaokoa watu wanaoonewa, Na macho ya kiburi utayadhili. |
28. | Kwa kuwa Wewe unaiwasha taa yangu; Bwana Mungu wangu aniangazia giza langu. |
29. | Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi, Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta. |
30. | Mungu, njia yake ni kamilifu, Ahadi ya Bwana imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote wanaomkimbilia. |
31. | Maana ni nani aliye Mungu ila Bwana? Ni nani aliye mwamba ila Mungu wetu? |
32. | Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu. |
33. | Miguu yangu anaifanya kuwa ya kulungu, Na kunisimamisha mahali pangu pa juu. |
34. | Ananifundisha mikono yangu vita, Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba. |
35. | Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kuume umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza. |
36. | Umezifanyizia nafasi hatua zangu, Na miguu yangu haikuteleza. |
37. | Nitawafuatia adui zangu na kuwapata, Wala sitarudi nyuma hata wakomeshwe. |
38. | Nitawapiga-piga wasiweze kusimama, Wataanguka chini ya miguu yangu. |
39. | Nawe hunifunga mshipi wa nguvu kwa vita, Hunitiishia chini yangu walioniondokea. |
40. | Naam, adui zangu umewafanya wanipe visogo, Nao walionichukia nimewakatilia mbali. |
41. | Walipiga yowe, lakini hakuna wa kuokoa, Walimwita Bwana lakini hakuwajibu, |
42. | Nikawaponda kama mavumbi mbele ya upepo, Nikawatupa nje kama matope ya njiani. |
43. | Umeniokoa na mashindano ya watu, Umenifanya niwe kichwa cha mataifa. Watu nisiowajua walinitumikia. |
44. | Kwa kusikia tu habari zangu, Mara wakanitii. Wageni walinijia wakinyenyekea. |
45. | Wageni nao walitepetea, Walitoka katika ngome zao wakitetemeka. |
46. | Bwana ndiye aliye hai; Na ahimidiwe mwamba wangu; Na atukuzwe Mungu wa wokovu wangu; |
47. | Ndiye Mungu anipatiaye kisasi; Na kuwatiisha watu chini yangu. |
48. | Huniponya na adui zangu; Naam, waniinua juu yao walioniinukia, Na kuniponya na mtu wa jeuri. |
49. | Basi, Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako. |
50. | Ampa mfalme wake wokovu mkuu, Amfanyia fadhili masihi |
← Psalms (18/150) → |