Psalms (150/150)    

1. Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.
2. Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3. Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4. Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;
5. Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6. Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.

  Psalms (150/150)