| ← Psalms (149/150) → |
| 1. | Haleluya. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Sifa zake katika kusanyiko la watauwa. |
| 2. | Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya, Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao. |
| 3. | Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa matari na kinubi wamwimbie. |
| 4. | Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu. |
| 5. | Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao. |
| 6. | Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao, Na upanga mkali kuwili mikononi mwao. |
| 7. | Ili kufanya kisasi juu ya mataifa, Na adhabu juu ya kabila za watu. |
| 8. | Wawafunge wafalme wao kwa minyororo, Na wakuu wao kwa pingu za chuma. |
| 9. | Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa; Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote. Haleluya. |
| ← Psalms (149/150) → |