| ← Psalms (143/150) → | 
| 1. | Ee Bwana, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu, Kwa uaminifu wako unijibu kwa haki yako. | 
| 2. | Wala usimhukumu mtumishi wako, Maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki. | 
| 3. | Maana adui ameifuatia nafsi yangu, Ameutupa chini uzima wangu. Amenikalisha mahali penye giza, Kama watu waliokufa zamani. | 
| 4. | Na roho yangu imezimia ndani yangu, Moyo wangu ndani yangu umesituka. | 
| 5. | Nimezikumbuka siku za kale, Nimeyatafakari matendo yako yote, Naziwaza kazi za mikono yako. | 
| 6. | Nakunyoshea mikono yangu; Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame. | 
| 7. | Ee Bwana, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni | 
| 8. | Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unijulishe njia nitakayoiendea, Kwa maana nakuinulia nafsi yangu. | 
| 9. | Ee Bwana, uniponye na adui zangu; Nimekukimbilia Wewe, unifiche. | 
| 10. | Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa, | 
| 11. | Ee Bwana, unihuishe kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni; | 
| 12. | Kwa fadhili zako utawakatilia mbali adui zangu; Na kuwaangamiza wote wanitesao nafsi, Kwa maana mimi ni mtumishi wako. | 
| ← Psalms (143/150) → |