| ← Psalms (142/150) → |
| 1. | Kwa sauti yangu nitamlilia Bwana, Kwa sauti yangu nitamwomba Bwana dua. |
| 2. | Nitafunua mbele zake malalamiko yangu, Shida yangu nitaitangaza mbele zake. |
| 3. | Nilipozimia roho uliyajua mapito yangu; Katika njia niendayo wamenifichia mtego. |
| 4. | Utazame mkono wa kuume ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho. |
| 5. | Bwana, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katika nchi ya walio hai. |
| 6. | Ukisikilize kilio changu, Kwa maana nimedhilika sana. Uniponye nao wanaonifuatia, Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi. |
| 7. | Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu. |
| ← Psalms (142/150) → |